Isaiah 40:22-28

22 aAnakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,
nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.
Huzitandaza mbingu kama chandarua,
na kuzitandaza kama hema la kuishi.
23 bHuwafanya wakuu kuwa si kitu,
na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.
24 cMara baada ya kupandwa,
mara baada ya kutiwa ardhini,
mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,
ndipo huwapulizia nao wakanyauka,
nao upepo wa kisulisuli
huwapeperusha kama makapi.

25 d“Utanilinganisha mimi na nani?
Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu.
26 eInueni macho yenu mtazame mbinguni:
Ni nani aliyeumba hivi vyote?
Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine
na kuziita kila moja kwa jina lake.
Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,
hakuna hata mojawapo inayokosekana.

27 fKwa nini unasema, ee Yakobo,
nanyi ee Israeli, kulalamika,
“Njia yangu imefichwa Bwana asiione,
Mungu wangu hajali shauri langu?”
28 gJe wewe, hufahamu?
Je wewe, hujasikia?
Bwana ni Mungu wa milele,
Muumba wa miisho ya dunia.
Hatachoka wala kulegea,
wala hakuna hata mmoja
awezaye kuupima ufahamu wake.
Copyright information for SwhNEN